Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro ameongoza zoezi la kuwavalisha vyeo maofisa wa polisi 747 waliohitimu mafunzo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi mkoani Dar es Salaam.

Akitoa taarifa za mafunzo hayo, mkuu wa chuo hicho, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa amesema kuwa wanafunzi 756 katika vyeo vya ukaguzi walianza mafunzo hayo yaliyofunguliwa Juni 18, 2021.

Mambosasa amesema kuwa wanafunzi 9 wameshindwa kuhitimu kwa sababu mbalimbali ambapo mmoja hakufaulu kwa sababu wakati wa mitihani alikuwa nje ya chuo kiofisi na hivyo ameelekeza apewe mtihani maalum.

Amesema kati ya nane waliobaki, mmoja alifariki dunia wakati wa mafunzo, wanne waliachishwa kutokana na utovu wa nidhamu, mmoja aliacha kazi hivyo kupoteza sifa mwingine kwa sababu za kiafya.

Kati ya waliohitimu, maofisa sita wamefanya vizuri zaidi katika masomo ya darasani, medani za kivita na kwata na gwaride.

@Tbc Taifa

Mtanzania ashinda mashindano ya ubunifu nchini Finland
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba Disemba 12, 2021