Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza siku tatu za maombolezo Nchini humo kufuatia vifo vya Mawaziri wawili waliofariki ndani ya siku moja January 12,2021 kwa kuugua Covid 19.

Waziri wa habari wa Malawi, Gospel Kazako amethibitisha kuwa Waziri wa Serikali za Mitaa, Lingson Belekanyama na Waziri wa Uchukuzi Muhammad Sidik Mia wamefariki Dunia ndani ya saa mbili tofauti.

“Bendera zote zitapepea nusu mlingoti kwa siku tatu kwa heshima ya Mawaziri hawa na Wamalawi wote waliofariki kwa Corona”.

Itakumbukwa katika hotuba ya Rais Chakwera aliyoitoa kwa njia ya radio alishauri taifa ktoingiza siasa katika janga hili badala yake wananchi wafanye kazi kukabili tishio dhidi ya wote linalotokana na virusi vipya vya Corona.

Vikao vya kamati za bunge kuanza January 18
Chadema yakana kufungua kesi ICC

Comments

comments