Wakulima  zaidi ya 4,000 wanatarajia kunufaika na maonyesho yakilimo biashara ambayo yatahusisha mikoa ya Nyanda za Juu Kusini,lengo kuu likiwa ni kuwasaidia wakulima kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maonyesho hayo, mtafiti wa mazao ya mahindi,maharagwe na soya ambaye ni mratibu wa maonyesho hayo, Leonard Sabula, amesema maonesho hayo yatafanyika kwenye mashamba ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kituo cha Uyole Mei, 2021 na wakulimawapatao 4,000 wanarajiwa kushiriki.

“Maonyesho ya awamu hii yatakuwa ya aina yake maana tumefanya maboresho makubwa nakuwahusisha wadau wengi, hadi sasa kampuni zaidi ya 20 zikiwamo za pembejeo za kilimo na biasharazimethibitisha kushiriki, nina imani wakulima watajifunza masuala mbalimbali ya kuongeza thamani katika mazao yao pia kupata masoko ya uhakika,” amesema Sabula.

Ameeleza kuwa kwa mwaka huu walishindwa kufanya maonyesho hayo kutokana na uwapo wamlipuko wa ugonjwa wa virusi vya corona, ambao ulisababisha maandalizi kukwama kutokana nawadau kulalamikia ukata wa fedha.

Sabula amebainisha kuwa maonyesho ya mwaka jana wadau 698 walishiriki wakiwamo wanaume 371 nawanawake 327, ambao walijifunza mbinu mbalimbali za kilimo bora.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TARI Kituo cha Uyole, Dk. Tulole Bucheyeki, aamesema maonyesho ya kilimo biashara yanalengo la kuongeza mnyororo wa thamani kwenye mazao.

Aidha amesisitiza kuwa kupitia maonyesho hayo wadau wanapata fursa ya kuonyesha teknolojia zao kupitia mashamba darasa  au vipando vya  aina mbalimbali za mazao waliyoyapanda, ambayo wanatumia kuwafundisha wakulima wanaotembelea.

Aron Kalambo: Mpigaji alikuwa fundi katika pigo lile
Serikali ya Kenya yatishia kuwafukuza kazi wahudumu wa afya