Mapacha tisa waliovunja rekodi ya Guiness Duniani kwa kuzaliwa kwa wakati mmoja na kuishi wamerejea salama nchini kwao Mali, ambao hapo awali walikuwa wakiishi katika eneo la matibabu jijini Casablanca nchini Morocco, tangu waondoke katika Zahanati waliyozalia Mei 4, 2021. 

Wazazi na watoto wao tisa walifika katika uwanja wa ndege katika mji mkuu, Bamako, hii leo Desemba 13, 2022 na kukaribishwa na Waziri wa Afya, Diéminatou Sangaré.

Bi Cissé (mama wa natoto hao) akiwa na watoto wake. Picha ya Guiness World Record.

Watoto hao wasichana watano na wavulana wanne – walitungwa mimba kwa kutumia matibabu ya urutubishaji katika mfumo wa uzazi (IVF) na walizaliwa kwa kupitia upasuaji.

Waziri wa Afya wa Mali, amesema, watoto hao walizaliwa wakiwa na wiki 30 na uzito wa kati ya gramu 500 na kilo moja (1.1lb na 2.2lb) ambapo kabla ya kujifungua Mei 4, 2021, Bi Cissé (mama wa natoto hao), alisafirishwa hadi Morocco na Serikali ya Mali kwa uangalizi maalum.

Wengine watano wafariki katika maandamano
Upandaji wa nauli: Polisi yaonya mawakala wa mabasi