Watoto 9 waliozaliwa kwa wakati mmoja Mapacha wa kipekee, wanasherehekea siku yao ya kuzaliwa kwa mara ya kwanza wakiwa katika hali ya afya tele na kuendela na hatua za ukuaji.
Baba wa mapacha hao Abdelkader Arby, ameambia ameongea na shirika la habari la BBC na kusema kwa namna ambavyo wamekuwa wakifurahia uwepo wa mapacha hao na ukuaji wao ukiwa wa kawaida.
“Sasa wanatambaa. Wengine wanaketi na hata kutembea wakijishikilia mahali,” alisema Abdelkader Arby, afisa wa jeshi la Mali.
Bado wako katika uangalizi wa kliniki nchini Morocco walikozaliwa, alisema. “Mama yao Halima Cissé, 26, pia anaendelea vyema.”
“Sio rahisi lakini twamshukuru Mungu. Hata kama inachosha wakati mwingine,unapowaona watoto wote wakiwa na afya njema, kutoka kulia kwenda kushoto tunafarijika. Tunasahau kila kitu,”alisema Arby.
“Ndio amerejea nyumbani kutoka Morocco kwa mara ya kwanza ndani ya miezi sita, akiwa na mtoto wake wa kwanza, Souda, mwenye umri wa miaka mitatu, Nafurahi sana kujumuika na familia yangu, mke wangu, watoto.”
Watakuwa na sherehe ndogo tu ya kuzaliwa wakiwa na wauguzi na watu wachache kutoka kwa jengo lao la ghorofa, Bw Arby alisema na kuongeza Kuwa hakuna kilicho bora kuliko mwaka wa kwanza. Tutakumbuka wakati huu mzuri tunaoenda kuupata.”
Kuzaa watoto wengi ni hatari na akina mama walio na zaidi ya vijusi wanne kwa wakati mmoja wanashauriwa kuavya mimba hiyo hasa katika nchi ambazo utoaji mimba ni halali.
Pia kuna hatari ya watoto kupata matatizo ya kiafya kutokana na kuzaliwa kabla ya wakati wao, kama vile sepsi s(kuvimba tishu na viungo) na kupooza kwa ubongo.
Bi Cissé na watoto hao kwa sasa wanaishi katika kile ambacho baba yao alikitaja kama “gorofa yenye tiba” ambayo ni ya wamiliki wa kliniki ya Ain Borja huko Casablanca ambako watoto hao walizaliwa.
“Kuna wauguzi ambao wako hapa, pamoja na mke wangu, ambao husaidia kutunza watoto, Kliniki imewapa menyu ambayo inasema nini cha kuwapa kula wakati wote, usiku na mchana,” aliendelea kuongea Arby.
Watoto hao ambao wasichana ni watano na wavulana wanne walizaliwa wakiwa na wiki 30 kulingana Waziri wa Afya wa Mali, Fanta Siby. Walikuw ana uzani wa kati ya gramu 500 na kilo moja (1.1lb na 2.2lb), Profesa Youssef Alaoui, mkurugenzi wa matibabu wa kliniki ya Ain Borja clinic aliambia shirika la habari la AFP wakati wa kuzaliwa kwao na Walizaliwa kupitia njia ya upasuaji.
Wavulana wanaitwa Mohammed VI, Oumar, Elhadji, Bah, nao wasichana wakapewa majina ya Kadidia, Fatouma, Hawa, Adama na Oumou na Kila mmoja wao ana kitu cha kipekee, baba yao alisema.
“Wate wana tabia tofauti. Wengine ni wapole, huku wengine wakipiga kelele na kulia sana. Wengine wanataka kuokota kila wakati. Wote ni tofauti sana, jambo ambalo ni la kawaida kabisa.”
“Serikali ya Mali ilitayarisha kila kitu kwa ajili ya matunzo na matibabu ya watoto hao tisa na mama yao. Sio rahisi hata kidogo, lakini ni nzuri na ni jambo la kufariji,” alisema.
Hawajafika Mali lakini tayari ni maarufu sana nchini humo, baba yao alisema.
“Kila mtu ana shauku kubwa ya kuwaona watoto kwa macho yao familia zao, marafiki, kijiji chetu, nchi nzima.”
Hata hivyo Arby ametoa ujumbe kwa wanandoa wanaojaribu kupata watoto, “Natumai Mungu atabariki kila mtu ambaye bado hajapata watoto – kwamba wanaweza kupata kile tulicho nacho sasa. Ni kitu kizuri, hazina halisi.”
Watoto hao walivunja Rekodi ya Dunia ya Guinness kwa kuwa watoto wengi zaidi kuzaliwa kwa wakati moja na kuishi na Kabla ya kujifungua mnamo Mei 4, 2021, Bi Cissé alisafirishwa hadi Morocco na serikali ya Mali kwa uangalizi maalum.