Maria na Consolata ambao ni mapacha walioungana wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa uchunguzi zaidi wa kiafya.

Mapacha hao ambao kwa sasa wanasoma chuo kikuu cha RUCO mkoani Iringa nchini Tanzania wanafanyiwa uchunguzi na jopo la madaktari watano ambao wameeleza kuwa mara baada ya uchunguzi huo wataweka wazi taarifa sahihi kuhusu matatizo yanayowasumbua mapacha hao.

Afisa uhusiano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Anna Nkinda amesema kuwa walimefikishwa hospitalini hapo wakiwa katika hali ya kawaida na wamefikishwa hapo kwa ajili ya uchunguzi wa matatizo ya moyo, hivyo kama kuna matatizo mengine tofauti na moyo watafanyiwa uchunguzi mwingine pia kuomba msaada wa madaktari wengine kama wakihitajika.

Vifo vingi hutokea wakati wa upasuaji Afrika
Mamlaka ya hali ya hewa yatoa angalizo