Mashambulizi makali ya ndege katika anga ya Syria yamesababisha vifo vya maelfu ya watu, siku moja tu baada ya Marekani na Urusi kutangaza kuwa vita katika nchi hiyo vitasitishwa mpaka siku ya Jumatatu.

Wakereketwa katika maeneo yaliyoshambuliwa wanasema kuwa watu 45 wameuawa katika makazi yaliyoshambuliwa na vitongoji vyake.

Katika mji unaokaliwa na waasi wa Idlib, ripoti zinasema watu wengine 40 waliuawa, kukiwemo wengi wao waliokuwa wakinunua mboga na matunda.

Serikali ya Syria na kundi kuu la upinzani linaloshiriki katika usuluhishi wa amani wameunga mkono mkataba huo ulioafikiwa mjini Geneva.

Iwapo mkataba huo wa amani utatekelezwa na kwa pane zote mbili  angalau wiki moja, Marekani na Urusi zinatarajia kushirikiana katika mashambulizi dhidi ya washambuliaji wa Kiislamu wenye itikadi kali

Shambulio La Kigaidi Latokea Katika Kituo Cha Polisi Mjini Mombasa na Kujeruhi Askari Kadhaa, Ulinzi Waimarishwa
Idadi Ya Maafa Yaliyotokana na Tetemeko La Ardhi Yazidi Kuongezeka