Mrembo Jokate Kidoti ameonesha kuwa na msimamo wa mapenzi na kazi baada ya kumuwekea ngazi nyingine Ali Kiba ili azidi kupandisha kuupeleka muziki wake Kimataifa.

Kidoti ambaye yuko na Ali Kiba jijini Nairobi, Kenya katika msimu wa tatu wa ‘Coke Studio Afrika’, ametumia nafasi hiyo kwa moyo wa mapenzi kumshawishi swahiba wake  Ice Prince kufanya collabo na Ali Kiba wakiwa jijini humo. Pendekezo lake lilikubaliwa na rapa huyo wa Nigeria ndani ya sekunde mbili.

“Forever My G. Ma Nig Fly Boi Choc Boi @iceprincezamani Leo Leo Video Loading. But First I Asked Him To Record A Song With Ali Like Tonite. He’s Like Lets Do This. LoL. #Tanzania #Nigeria #Afrika #Kidoti,”aliandika Jokate.

Kwa mujibu wa post hiyo, video ya wimbo wa ‘Leo Leo’ wa Jokate aliomshirikisha Ice Prince itakamilishwa hivi karibuni.

Ali Kiba amekutana pia na Ne-yo ambaye wamerekodi na kutumbuiza naye wakati wa kurekodi msimu wa ‘Coke Studio Afrika’.

Pedro: Nimefurahi Sana Kufika Hapa
Siri Yafichuka, Fàbregas Alikua Kibaraka Wa Mourinho