Siku mbili mara baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya amani baina ya waasi na serikali juu ya mgogoro uliodumu kwa takribani miaka 50 nchini Colombia, Rais wa nchi hiyo Juan Manuel Santos ametoa amri kwa jeshi kusimamisha mapigano dhidi ya kundi la waasi la Farc.

Rais Santos amesema mapigano yatasitishwa kuanzia usiku wa jumatatu,Farc walitangaza kusitisha mashambulizi mwaka mmoja uliopita.

Hata hivyo mbali na uamuzi wa serikali ya Colombia kusitisha mashambulizi dhidi ya waasi lakini imekataa kutoa taarifa rasmi za kijeshi mpaka makubaliano yatakapo kamilika ya mkataba wa makubaliano ya amani ambao bado unasubiri kupigiwa kura ya maoni na wananchi wa Colombia.

Mwanaume Mmoja Nchini India Abeba Maiti Ya Mkewe Mabegani Kwa Takribani Kilomita 12
Temeke Yaandaa Operesheni Stendi Ya Mbagala