Mapigano makali yameripotiwa kati ya vikosi vya polisi na waandamanaji nje ya kituo cha polisi jijini Cairo baada ya kutokea kifo cha kijana mmoja aliyekuwa rumande.

Taarifa zimesema kuwa waandamanaji hao wanalituhumu jeshi la polisi kwa kumtesa kijana huyo mpaka kusababisha kifo chake.

Aidha, waandamanaji hao wamechoma moto magari ya polisi, kuyapiga mawe na kujaribu kuchoma pia kituo cha polisi, ambapo jeshi hilo limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji hao na baadhi yao kuwakamata.

Hata hivyo, Kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja la Afroto alikamatwa siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya na polisi imesema kuwa alifariki baada ya kupigana na wafungwa wenzake.

 

Magazeti ya Tanzania leo Januari 7, 2018
Muisrael akamatwa kwa kuuza viungo vya Binadamu