Vita nchini Sudan, vimeingia mwezi wa tatu wakati idadi ya vifo ikifikia watu 2,000 na baada ya Gavana wa jimbo hilo kuuawa katika jimbo la Darfur.
Jeshi linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan limekuwa likipigana na vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces – RSF, vinavyoongozwa na aliyekuwa naibu wake, Mohamed Hamdan Daglo.
Mapigano hayo yamesababisha watu milioni 2.2 kuyakimbia makaazi yao, wakiwemo watu 528,000 ambao wamekimbilia nchi jirani, Tangu kuanza kwa mapigano hayo Aprili 15, 2023.
Mmoja kati ya raia zaidi ya milioni moja, ambao waliyakimbia mapigano hayo katika mji mkuu Khartoum, Mohamad al-Hassan alisema hatukutarajia kama vita hivyo vingeendelea kwa muda mrefu na kwamba hawajui iwapo watarudi au watalazimika kuanza maisha mapya.