Mashambulizi kutoka kwa makundi hasimu ya kabila la Dinka katika eneo linalozozaniwa na Sudan pamoja na Sudan Kusini, yamesababisha mauaji ya watu 32 mwishoni mwa juma.
Waziri wa Habari wa eneo la Abyei, Bulis Koch amesema kundi la vijana la Twic Dinka linaloungwa mkono na Wanamgambo wa ndani lilivishambulia vijiji vya Kabila la Ngok Dinka Kaskazini Mashariki mwa mji wa Agok.
Vita kama hivyo vimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini Sudan Kusini na Taifa hilo liliingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe muda mfupi baada ya Sudan kujipatia Uhuru wake mwaka 2011.
Hata hivyo, makubaliano ya amani yaliyosainiwa miaka mitatu iliyopita yanaendelea lakini Serikali ya mpito imekuwa ikishindwa kuunganisha makundi ya jeshi na kutengeneza umoja.