Mapigano kati ya Taliban na vikosi vya serikali ya Afghanistan yameanza tena mapema leo asubuhi katika jimbo la Helmand, baada ya kumalizika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku tatu. 

Makubaliano hayo yalifikiwa ili pande zote zinazohasimiana ziweze kusherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr. 

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha DW, Msemaji wa jeshi la Afghanistan na afisa wa eneo hilo wamesema kulikuwa na mapigano kwenye viunga vya Lashkar Gah, mji mkuu wa Helmand, ambao umeshuhudia mapigano yakiongezeka tangu Marekani ilipoanza kuyaondoa majeshi yake Afghanistan kuanzia tarehe moja ya mwezi huu wa Mei. 

Aidha, msemaji wa Taliban, Zabihullah Mujahid amesema vikosi vya serikali ya Afghanistan ndiyo vimeanzisha operesheni, hivyo kundi hilo lisilaumiwe. 

Makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku tatu yaliyoanzishwa na Taliban na kukubaliwa na serikali ya Afghanistan, yalimalizika jana usiku.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Mei 17, 2021
Rasmi wakuu wa mikoa kuapishwa Mei 19, 2021