.

Kuna hofu kubwa kuwa Sudan kusini huenda ikatumbukia tena kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mara baada ya kusikika kwa milio ya risasi katika mji muhimu wa Yei, kusini magharibi mwa Juba, kwenye barabara inayounganisha Juba na taifa jirani la Uganda.

Vikosi vikosi vya makamu wa rais, Riek Machar, vinasema kwamba vikosi vya serikali viliwashambulia katika maeneo yao siku ya jumamosi.

Mwezi uliopita vikosi  vyote vya rais Salva Kiir na Riek Machar vilishambuliana mjini Juba, ambapo mashambuliano hayo yaliifanya UN kuongeza wanajeshi 400 nchini humo kwaajiri ya kulinda kuhakikisha usalama.

Hata hivyo Bw Kiir amesema hataruhusu Umoja wa Mataifa kuchukua udhibiti wa nchi yake na hatashirikiana tena na umoja huo.

Uhasama wa kisiasa baina bwana Kiir na  Machar umesababisha mapigano tangu 2013,wawili hao waliweka saini ya mkataba wa amani mwaka 2015, japo mapigano ya mara kwa mara yamekuwa yakiendelea baina ya pande zote mbili.

Zaidi ya raia 100,000 wa Sudan kusini kwa sasa wamekimbilia katika nchi jirani kufuatia mapigano ya hivi karibuni, linasema shirika la la wakimbizi la Umoja wa Mataifa

Ziara Ya Jaffo Manispaa Ya Mpanda Yamuweka Matatani Afisa Mipango Miji
Waziri Wa Elimu Ajiuzulu Kwa Ulevi Sweden