Shughuli za kawaida na Safari za ndege, zimeanza tena katika mji mkuu wa Libya Tripoli baada ya mapigano kati ya wafuasi wa serikali zinazohasimiana na kusababisha vifo vya takriban watu 32 na kuzusha hofu ya kutokea mzozo mwingine.
Mapigano hayo, yametokea baada ya miezi kadhaa ya kuongezeka kwa mvutano kati ya wafuasi wa Abdulhamid Dbeibah na Fathi Bashagha, ambao tawala zao hasimu zinawania udhibiti wa nchi.
Utawala wa Dbeibah, uliosimikwa katika mji mkuu kama sehemu ya mchakato wa amani ulioongozwa na Umoja wa Mataifa mwaka jana 2021, ambao hadi sasa umemzuia Bashagha kuchukua madaraka, huku aksema kuwa utawala ujao unapaswa kuwa zao la uchaguzi.
Bashagha, aliteuliwa na bunge la Libya lililoko mashariki mwa nchi hiyo mapema mwaka huu, na aungwa mkono na kiongozi mwenye nguvu wa kijeshi Khalifa Haftar, ambaye jaribio lake la mwaka 2019 la kuuteka mji mkuu kwa nguvu liligeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka mzima.
Baadhi ya makundi yenye silaha, yanazingatiwa kutoegemea upande wowote katika mzozo wa hivi punde unaonga mkono wafuasi wa Dbeibah wikendi hii kuzima jaribio la pili la Bashagha kuingia mji mkuu.
Pande hizo mbili, zilitupiana lawama siku ya Jumamosi Agosti 29, 2022 huku mataifa yenye nguvu duniani yakiomba utulivu licha ya ghasia ambazo zimekuwa zikiendelea katika maeneo mbalimbali nchini humo.