Mapigano kati ya jeshi na wanamgambo nchini Sudan yamesababisha vifo vya takriban watu 200 na kujeruhi 1,800, kuharibu majengo ya Hospitali na kukwamisha misaada vita hivyo vinavyopiganwa mjini Khartoum.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amezitaka pande zinazopigana nchini Sudan kusitisha uhasama mara moja huku msafara wake ulielekea mjini Khartoum na kusema ongezeko la mzozo kati ya jeshi na makundi ya kijeshi, wakiongozwa na majenerali wapinzani, “unaweza kuleta athari kubwa nchini humo na katika eneo la kanda hiyo.
Vurugu hizo, ambazo zilizuka siku ya Jumamosi Aprili 15, 2023 zimekuwa zikiendelea kwa muda wa siku ya tatu hadi jana huku idadi ya vifo vya watu vikiongezeka hadi kufikia vifo wasiopungua 185, Volker Perthes, mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan, aliwaambia waandishi wa habari.
Mapigano hayo, yalizuka kufuatia vita vya kugombania madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021, Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na Makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo ambaye ni kamanda anayeongoza kikosi cha Rapid chenye nguvu.