Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya kibinadamu OCHA, imesema watu wapatao milioni 3 wamekimbia makazi yao nchini Sudan katika kipindi cha katikati ya mwezi April, 2023.

Shirika hilo, limeeleza kuwamba watu wengine zaidi ya 880,000 wamelazimika kukimbia na kwenda nje ya nchi na kwamba wakimbizi wengi wa Sudan wamekwenda Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Misri, Ethiopia na Sudan Kusini.

Aidha, OCHA ambalo ni Shirika hilo la Umoja wa mataifa imesema jumla ya watu milioni 20.3, sawa na asilimia 42 ya wakazi wa Sudan, wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

Hata hivyo, pia imesema hali katika eneo la magharibi la Darfur inatia wasiwasi kutokana na Jeshi la Sudan linaloongozwa na Kiongozi wa kijeshi Abdel Fattah Burhan kuwa katika mzozo wa kugombea madaraka na Wanajeshi wa kikosi cha Msaada wa Haraka – RSF, kinachoongozwa na makamu wake wa zamani Mohammed Hamdan Daglona.

Ligi Kuu Zanzibar rasmi Septemba 09
WHO yatahadharisha Dawa ya Kikohozi inayouwa