Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak kutoka Chama cha Conservative, amepoteza viti viwili muhimu vya bunge katika kura ya maoni ya kuashiria mwelekeo kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Chama cha Labour, kimefanikiwa kushinda kwa urahisi viti viwili vilivyokuwa wazi katikati mwa England katika uchaguzi mdogo uliofanyika Oktoba 19, 2023.
Hata hivyo, George Osborne, aliyekuwa mweka hazina wa zamani wa Conservative, alionya mapema kuwa kupoteza Mid Bedfordshire kunaweza kuwa na matokeo mabaya kwa chama cha kihafidhina.
“Haya ni matokeo ya kipekee. Kushinda katika ngome hizi za Conservative kunathibitisha kuwa watu kwa kiasi kikubwa wanataka mabadiliko na wako tayari kuweka imani yao kwa Chama chetu cha Labour kilichobadilika ili kuyatekeleza,” alisema Starmer.
Hata hivyo, tangazo la sera hizo halijachangia sana kuboresha hali ya Conservatives katika kura, ingawa umaarufu binafsi wa Sunak umepanda kidogo.
Katika miaka zaidi ya 13 walipokuwa madarakani, Conservatives wameiongoza Uingereza kupitia baadhi ya matukio muhimu zaidi kwa miongo, ikiwa ni pamoja na Brexit na janga la COVID-19.
Sunak, kiongozi wa tano wa Conservative tangu mwaka 2010, hakuwepo Uingereza wakati wa matokeo ya uchaguzi mdogo baada ya kusafiri kwenda Israel kutoa msaada kwa nchi hiyo katika vita vyake na kundi la Hamas.