Umoja wa Afrika – AU, umesitisha ushiriki wa Gabon katika shughuli zake zote, kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa Rais Ali Bongo madarakani.
Uamuzi huo, umekuja baada ya mkutano wa hapo jana Agosti 31, 2023 wa Baraza la Amani na Usalama la umoja huo, huku Wanajeshi wa Gabon wakimtangaza Mwanajeshi mwenzao, Jenerali Brice Nguema kuwa Kiongozi wa mpito.
Aidha, Wanajeshi hao hata hivyo hawakutoa maelezo zaidi juu ya muda gani utakuwa wa mpito na lini utawa wa Serikali ya kiraia utarejeshwa.
Hata hivyo, Muungano Mkuu wa Vyama vya Upinzani umewataka watawala hao kujadili njia bora zaidi za kumaliza mzozo huo.