Mataifa ya Afrika ya Magharibi yamesitisha mkutano muhimu wa kijeshi juu ya mzozo wa Niger, ikiwa ni siku moja baada ya kusema wangetuma kikosi cha kumrejesha madarakani kiongozi wa nchi hiyo aliyepinduliwa, Mohamed Bazoum.
Wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Magharibi – ECOWAS, walikuwa wakutane hii leo Agosti 12, 2023 katika mji mkuu wa Ghana Accra, lakini tamko la kuuakhirisha mkutano huo kwa muda usiojulikana limetolewa.
Vyanzo hivyo, vilisema mkutano huo ulikuwa umeandaliwa ili kuwaeleza viongozi wa ECOWAS juu ya njia bora zaidi za kuunda na kutuma kikosi hicho cha dharura nchini Niger huku .
Hata hivyo, ECOWAS haijafafanuwa undani wa kikosi hicho wala ratiba ya hatua zake, huku viongozi wake wakisisitiza kuwa wanataka suluhisho la amani na maelfu ya wananchi wa Niger walikusanyika kuunga mkono jeshi lao mbele ya kituo kimoja cha jeshi.