Takribani watu 160 wamefariki dunia kutokana na maporomoko ya theluji katika nchi za Pakistan na Afghanistan huku hali ya hewa ikielezwa kuzidi kuwa mbaya.
Kikosi cha Uokozi Nchini Pakistan kimepata miili ya watu 21 waliopoteza maisha kutokana na Maporomoko ya theluji katika Jimbo la Kashmir na kuifanya idadi ya waliopoteza maisha nchini Pakistan na Afghanistan kufikia 160.
Eneo lililoathirika zaidi ni la Kashmir ya Upande wa Pakistan, hususan bonde la Neelum.
Waziri wa Huduma za Dharura wa Pakistan, Ahmad Raza Qadri amesema tangu Jumapili, kumekuwa na hali mbaya ya hewa iliyosababisha vifo 76 katika Jimbo la Kashmir na wengine 45 wameuawa katika Jimbo la Baluchistan Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.