Uongozi wa klabu ya Young Africans umethibitisha itafanya usajili wa nyota wanne wa kigeni mwishoni mw amsimu huu, kufuatia mapendekezo ya kocha Luck Eymael.
Mkuu wa idara ya habari na mawasilino wa Young Africans Hassan Bumbulia amesema, kabla ya kocha Aymael hajaondoka juma lililopita, aliwasilisha ripoti ya maboresho ya kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao
“Mwalimu alituachia ripoti yake ya usajili ambayo tayari wadhamini wetu kampuni ya GSM wameanza kuifanyia kazi,” amesema Bumbuli
“Mwalimu anahitaji wachezaji wanne wa kigeni wanaocheza nafasi za beki, kiungo, winga na mshambuliaji, Pia amependekeza wachezaji ambao mikataba yao imemalizika lakini anahitaji kuwa nao msimu ujao”
“Tunaendelea na mazungumzo na wachezaji wanane ambao mikataba yao ipo ukiongoni”
Wakati huo huo, Kocha Luc Eymael anatarajiwa kurejea nchini siku za karibuni ili kuwahi mikiki mikiki ya ligi kuu inayotarajiwa kuendelea baada ya April 17.
Eymael aliruhusiwa kwenda kwao ambapo juma lililopita alifunga ndoa nchini Afrika Kusini na kisha alielekea Ubelgji.
Kocha huyo atakaporejea atakaa karantini kwa muda wa siku 14 kulingana na agizo la Serikali kwa wageni wote wanaoingia nchini, na baadae ataanza maandalizi ya kikosi chake kabla ya kuendelea kwa ligi kuu na michuano ya kombe la shirikisho (ASFC).
Hivi karibuni Eymael alikaririwa na vyombo vya habari akisema, kwa sasa hafikirii ubingwa wa ligi kuu kwani tayari wamepoteza nafasi ya kushinda taji hilo, hivyo ataweka kipaumbele kwenye michuano ya kombe la shirikisho (ASFC), ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya Kimataifa msimu ujao.