Gwiji wa soka nchini Argentina, Diego Armando Maradona Franco amemshauri nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Lionel Messi kwa kumwambia anapaswa kuwa na moyo wa kizalendo na kutokatishwa tamaa na mambo mdogo katika soka lake.

Maradona, amelazimika kumueleza ukweli Messi baada ya kushuhudia mzozo ukichukua nafasi kubwa miongoni mwa wadau wa soka nchini Argentina ambao umekua ukielekezwa kwa mshambuliaji huyo kufuatia muonekano aliouonyesha mara baada ya timu yao ya taifa kushindwa katika hatua ya fainali kwenye michuano ya Copa America, kwa kufungwa na Chile kwa mikwaju ya Penati.

Gwiji huyo amesema pamoja na yote hayo kujitokeza bado mshambuliaji huyo anapaswa kuwa na moyo wa kizalendo kwa kuamini anazungumzwa kutokana na mapungufu yaliyojitokeza lakini ubora wake utaendelea kusimama.

Hata hivyo Maradona mwenye umri wa miaka 54, amewataka mashabiki wa soka nchini Argentina kuonyesha heshima dhidi ya Messi, kutokana na jitihada zake ambazo amekua akizionyesha kila kukicha kwa lengo la kuisaidia timu yao ya taifa na kinachotokea uwanjani pale timu inapofanya vibaya ni bahati mbaya kwao wote.

Amesema hakuna shabiki wa soka kutoka nchini Sweden atakeishangilia Argentina, zaidi ya wananchi wa Argentina kupenda cha kwao wenyewe na si kuangalia nani ni kikwazo cha kushindwa kuwasaidia wanapokua katika mazingira magumu.

Wadau wa soka nchini Argentina wamekua wakimnyooshea vidole Lionel Messi kwa kumtuhumu ameshindwa kufanya lolote la maana, kwa kuisaidia timu yake ya taifa, tofauti na anavyokua katika klabu yake ya Barcelona ambapo mara kadhaa amekua akionyesha juhudi za kuiwezesha klabu hiyo ya nchini Hispania kutwaa mataji makubwa barani Ulaya.

CUF Wazungumzia Taarifa Za Kujitenga Na UKAWA
Mlengwa Katika Usajili Wa Arsenal Apata Majanga