Nguli wa soka nchini Argentina na ulimwenguni kwa ujumla Diego Maradona, amejitokeza na kumtetea Lionel Messi, kwa kusema mchezaji huyo hana haja ya kudhihirisha yeye ni bora katika mashindano ya kombe la dunia yatakayofanyika Urusi mwezi Juni.
Amesema hayo kufuatia kukusolewa na wadau mbalimbali wa soka kwa kushindwa kuisaidia timu ya taifa kwenye michuano mikubwa.
Messi anajipanga kuiongoza Argentina kuchukua ubingwa wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka huu, Mshindi huyo mara tano kwenye tuzo za Ballon d’Or hajawahi kushinda taji lolote kubwa akiwa na timu ya taifa, mwaka 2014 Argentina ilipoteza mchezo wa fainali mbele ya Ugerumani katika mchezo wa fainali za kombe la dunia zilizofanyika nchini Brazil.
-
Ngorongoro Heroes waichapa Msumbiji
-
Welayta Dicha kuamua safari ya Young Africans
-
Nyota wa Tenesi nchini Uingereza kuwania ubingwa wa Malkia
‘’Ningependa kumshauri Messi kuendelea kucheza,na kufurahia mchezo” amesema Maradona. ‘’inabidi asahau kuhusu kukosolewa,kama atashinda au hata shinda kombe la dunia haitaji kuthibitisha chochote ,inabidi afurahie mchezo ndani ya uwanja’’ ameongeza Maradona.
Aidha,Messi ameisadia Argentina kufuzu fainali hizo za kombe la dunia zitakazo fanyika nchini Urusi kwa kufunga mabao matano yakiwemo mabao matatu aliyo yafunga katika mchezo dhidi ya Ecuador.