Uongozi wa Klabu ya Borussia Dortmund, una mpango wa kumpatia mkataba mpya Kiungo na Nahodha wap, Marco Reus ili kubakisha kwenye kikosi cha klabu hiyo.
Reus anatarajiwa kupewa mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuwa hapo huku mshahara wake ukiboreshwa mpaka kufikia Euro Milioni 7 kwa mwaka.
Nyota huyo ambaye ni nahodha wa kikosi hicho ni moja kati ya wakongwe ambao wamebaki kama alama ndani ya Borussia Dortmund.
Reus anatarajiwa kupewa mikataba mpya kikosini hapo wakati wowote kabla ya msimu huu kumalizika.
Borussia Dortmund tayari imefanikiwa kumuongeza mkataba nyota wake Julian Brandt ambaye amesaini mkataba mpya ambao utamuweka ndani ya kikosi hicho hadi Juni 2026.
Dortmund kwa sasa kuelekea mwisho wa msimu inapamnbana kuweka sawa mambo ya mikataba kwa wachezaji wake.