Meneja wa klabu ya Olympiacos, Marco Silva ameahidi kuweka historia katika uwanja wa Emirates kwa kuifunga The Gunners nyumbani.

Silva amesema kikosi cha klabu ya Olympiacos hakijawahi kushinda katika uwanja wa Emirates uliopo kaskazini mwa jijini London, na wakati wote wa safari alikua akitia nia ya kwenda ugenini kufanya maajabu na kuwaacha wenyeji wakuwa katika hali ya taharuki.

Amesema ni vigumu kwa walio wengi kumini kama suala hilo inawezekana, lakini ukweli wa mambo anaujua yeye mwenyewe ambaye amesisitiza kuisoma Arsenal na kujua mapungufu yao.

Menaja huyo kutoka nchini Ureno amesema, maandalizi mazuri aliyofanya kikosini mwake, yanampa jeuri ya kutangaza ushindi kuelekea katika mchezo huo na hana shaka na kauli aliyoitoa.

Arsenal kwa mara ya mwisho waliwafunga Olympiacos mabao matatu kwa moja miaka mitatu iliyopita, hali ambayo iliendelea kudhihirisha mabingwa hao wa nchini Ugiriki wameshindwa kujizatiti mbele ya The Gunners kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Olympiacos wamesafiri hadi jijini London, huku wakichagizwa na matokeo amzuri ya kushinda michezo yote ya nyumbani msimu huu, lakini bado wanasumbuliwa na rekodi ya kushinda wanapokua kwenye ardhi ya nchini England baada ya kupoteza michezo yao 12 waliyowahi kucheza.

Olympiacos wamewahi kucheza dhidi ya Manchester United, Chelsea, Newcastle, Arsenal pamoja na Liverpool.

Mchezo mwingine wa kundi F utakaochezwa hii leo utakua kati ya mabingwa wa soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich dhidi ya mabingwa wa soka nchini Croatia Dynamo Zagreb.

Michezo ya makundi mengine itakayochezwa leo.

Champions League – Kundi la 5

BATE Borisov VS Roma

Barcelona VS  Bayer Leverkusen

 

Champions League – Kundi la 7

FC Porto VS Chelsea

Maccabi Tel Aviv VS Dynamo Kyiv

 

Champions League – Kundi la 8

Lyon VS Valencia

Zenit St. Petersburg VS FC Gent

Shamsa Ford Azikataa Fedha Za Chama...
Arsenal Kujaribu Bahati Ya Pili Ulaya