Balozi wa Ufaransa Nchini Niger, Sylvain Itté hatimaye ameondoka Niamey kuelekea Ndjamena, Mji Mkuu wa Chad, ambapo mwanadiplomasia huyo ataanzisha safari yake kwenda jijini Paris.

Kuondoka huko kunaashiria mwisho wa wiki kadhaa za mvutano kati ya Paris na Uongozi wa Kijeshi unaoshikilia madaraka Nchini Chad, tukio ambalo linakuja siku chache baada ya Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron akutangaza kuwa Balozi Itté ataondoka nchini Niger hivi karibuni. 

Balozi wa Ufaransa Nchini Niger, Sylvain Itté.

Utawala huo wa kijeshi, Agosti 2023 ulitangaza kutomuhitaji Balozi huyo wa Ufaransa na tangu wakati huo, Sylvain Itté amekuwa akiishi pamoja na maafisa sita wa timu yake ya ubalozi bila kujua hatma yao.

Macron kupitia mahijiano aliyoyafanya na kituo kimoja cha Luninga. alisema Balozi Sylvain Itté alishikiliwa “mateka” na jeshi lililoko madarakani, huku likizuia balozi huyo na Wasaidizi wake kupeawa chakula.

Bilioni 80 za REA kutekeleza miradi ya Umeme Kagera
Wataalam wazindua utafiti uhamaji wa hali ya hewa