Taarifa zinaeleza kuwa, beki wa pembeni wa klabu ya Fiorentina Marcos Alonso Mendoza, amefanyiwa vipimo vya afya jijini Londona muda mchache uliopita na wakati wowote anatarajia kutambulishwa kama mchezaji halali wa klabu ya Chelsea.

Inasemekana ada ya iliyokubaliwa na viongozi Fiorentina kwa ajili ya uhamisho wa beki huyo mwenye umri wa miaka 25 ni Euro milioni 23.

Kituo cha Sky Sports kimeripoti kuwa, Alonso aliwasili jijini London mapema hii leo na kisha alifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha taratibu nyingine za uhamisho wake.


Ushahidi mwingine ambao unatajwa kuthibitisha mchezaji huyo atakuwa miongoni mwa watakaounda kikosi cha Antonio Conte ni hatua yake ya kuanza kuifuata akaunti ya twitter ya klabu ya Chelsea.

KRC Genk Yamuachia Mbwana Samatta Kwa Masharti
Moussa Sissoko Arejea England, Spurs Wahusishwa