Mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford, huenda akaukosa mchezo wa Mkondo wakwanza wa Robo Fainali Ligi ya Europa dhidi ya Sevilla utakaochezwa keshokutwa Alhamis (April 13).
Taarifa zinaripoti kuwa Benchi la Ufundi la Manchester United linasubiri uhakika kutoka kwa madaktari kuhusu hali ya Mshambuliaji huyo aliye katika kiwango bora msimu huu 2022/23.
Rashford alipata maumivu ya misuli wakati wa mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Everton, ambao ulishuhudia Mashetani Wekundu wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Inaaminika Rashford alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyonga na huenda akakaa nje ya dimba kwa muda wa majuma matatu, lakini taarifa ya vipimo itaainisha kwa undani.
Michezo mingine ya Europa League Robo Fainali.
Juventus vs Sporting CP
Feyenoord vs Sevilla
Bayer Leverkusen vs Royale Union Saint-Gilloise