Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Democrat cha nchini Marekani Joe Biden amemteua Seneta wa Califonia Kamala Harris kuwa mgombea mwenza kwenye kinyang’anyiro hicho.
Aidha hatua hiyo inaandika historia mpya nchini Marekani kwa mwanamke huyo mweusi na raia wa kwanza mwenye asili ya Marekani na asia kugombea nafasi yenye wadhifa wa juu katika kinyang’anyiro cha Urais.
Harris ameandika kupitia mtandao wake wa twitter baada ya kuteuliwa akisema anajisikia heshima kuungana na Biden na amekubali kufanya kila liwezekanalo kumsaidia kuwa amiri jeshi kuu
Harris alikuwa karibu n mtoto wa Biden Beau, aliyekuwa mwanasheria mkuu katika jimbo la Delaware, na yeye akiwa na wadhifa kama huo katika jimbo la California
‘Huko nyuma wakati Kamala akiwa mwanasheria mkuu alifanya kazi karibu na Beau niliona namna walivyoshirikiana kuyashughulikia mabenki makubwa kunyanyua mazingira ya wafanyakazi na kuwalinda wanawake na watoto kutoka kwenye unyanyasaji nilifurahia sana na ninayo heshima sasa kuwa na yeye kama mwenzangu katika kampeni hii’. Amesema Biden.