Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya kimataifa yaliyopelekea Iran kuondolewa vikwazo vya kibiashara kwa kukubali kusitisha mpango wake wa nyuklia.

Rais huyo wa Marekani amesema kuwa Iran inapaswa kuendelea kuwekewa vikwazo dhidi ya mpango wake wa utengenezaji wa silaha za nyuklia ambao ameuita ni hatari kwa usalama wa dunia.

“Leo hii ninatangaza mkakati wetu pamoja na hatua kadhaa tutakazozichukua kuhakikisha Iran kamwe kamwe haitengenezi silaha za nyuklia. Kuna haja gani ya kuwa na makubaliano ambayo uwezo wake mkubwa ni kuchelewesha tu mpango wa nyuklia wa Iran kwa muda mfupi?” amesema Trump

Aidha, Trump ameliachia Bunge la Congress kufanya maamuzi ya mwisho kwani Wabunge wana siku 60 za kuamua kama wanataka kuiwekea tena vikwazo vya kibiashara Iran ama kutoiwekea.

Hata hivyo, kwa upande wake Rais wa Iran, Hassan Rouhani amesema kuwa masuala yote muhimu yanayoweza kujitokeza hayatoweza kushughulikiwa ikiwa mkataba huo utavunjwa, kwa sababu makubaliano hayo yanaondoa hatari kubwa sana, siyo tu hatari ya mashindano ya kuunda silaha za nyuklia katika kanda hiyo, lakini pia kuenea kwa nyuklia kusikodhibitiwa.

Polepole: Mgombea ubunge sharti awe mkazi wa jimbo analowakilisha
LIVE: Rais Magufuli katika maadhimisho ya Nyerere Day na Kilele cha Mwenge wa Uhuru Zanzibar