Marekani imetangaza mpango wa kurejea katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni miaka mitatu tangu Rais wa zamani, Donald Trump alipoitoa nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema kuiondoa Marekani Juni 2018, hakukusaidia kuleta mabadiliko yoyote ya maana ila kulisababisha ombwe la Uongozi ambalo Mataifa yenye ajenda za kimabavu yamelitumia kwa faida yao.
Uamuzi huo unaweza kukosolewa na Wabunge na raia wanaoiunga mkono Israel, ambao wamelikosoa Baraza hilo kwamba halichukulii kwa uzito ukiukaji wa Tawala na Serikali za Kimabavu, na linazikubali nchi husika kuwa wanachama.