Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameunganisha mpango wake wa kupambana na janga la virusi vya Corona katika siku zake 100 za mwanzo za urais huku akiahidi kwamba serikali yake itatoa chanjo milioni 100 kote nchini humo.
Kwenye kikao kilichofanyika Wilmington, Delaware, Biden amesema kuwa ataliomba Bunge kuruhusu ufadhili kamili wa mchakato wa kusambaza chanjo kote nchini humo.
Ameongeza kuwa katika siku 100 za mwanzo za urais wake, kwa pamoja wataweza kubadilisha mkondo wa ugonjwa huo nchini humo lakini pia hali ya Wamarekani.
Biden ambaye pia aliitambulisha timu yake ya afya ya umma, amesema kuwarejesha watoto shuleni, ni suala ambalo serikali yake italipatia kipaumbele.
Takriban watu 283,000 wamefariki nchini humo kutokana na uginjwa wa Covid 14 na mamilioni wamepoteza ajira.
Hapo jana Mamlaka ya dawa na chakula ya Marekani ilichapisha waraka kuhusiana na usalama na uthabiti wa chanjo ya Pfizer Inc’s ambayo huenda ikapata idhini ya dharura mwezi huu kutumika Marekani.