Marekani inatarajia kuanza kufanya majaribio ya kutungua makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kusafiri kutoka bara moja hadi jingine kwaajili ya kujihakikishia usalama.
Jeshi la nchi hiyo limesema kuwa jaribio hilo litakuwa maalum kwaajili ya kujikinga na makombora ya masafa marefu ambapo jaribio hilo linatarajiwa kuanza kufanyika wiki ijayo.
Marekani imefikia hatua hiyo mara baada ya wasiwasi mkubwa kutanda kuhusu uboreshaji miradi ya silaha za nyuklia na makombora ya masafa marefu wa Korea Kaskazini ambao umekuwa ukipigiwa kelele.
Aidha, Mkuu wa shirika la ujasusi la Marekani amesema kuwa iwapo miradi ya Korea Kaskazini ya kutengeneza makombora haitodhibitiwa, basi taifa hilo lina uwezo wa kutengeneza kombora lenye uwezo mkubwa kuliko yote duniani.
Hata hivyo Marekani imeonekana kuwa wasiwasi mkubwa kuhusu mpango wa Korea Kaskazini wa kutengeneza makombora mbali na mpango wake wa Kinyuklia, ambapo nchi hiyo imedai mpango ni kwaajili ya kujilinda.