Baraza la wawakilishi la Marekani limepiga kura kuweka vikwazo vipya dhidi ya Urusi, Iran na Korea Kaskazini kufuatia kukiuka baadhi ya makubaliano ambayo walijiwekea ya kuhakikisha wanalinda amani na usalama katika maeneo husika.
Urusi inawekewa vikwazo kutokana na kudaiwa kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka jana wa Marekani huku Korea Kaskazini na Iran wao wakiwekewa vikwazo kufuatia kufanya majaribio ya makombora ya nyuklia.
Aidha, Muswada huo unatarajiwa kupitia kwa baraza la seneti kabla ya kupelekwa kwa Rais Trump ili aweze kuidhinisha na kuwa sheria kamili ambayo itatumika kuzishughulikia nchi hizo kwa kukiuka taratibu za makubaliano.
Baadhi ya wawakilishi kutoka chama cha Democratic na Republican wamesema kuwa zinahitajika kuchukuliwa hatua kali dhidi ya Urusi kwani hawawezi kuivumilia nchi hiyo kuingilia uchaguzi wao japo Rais wao anapinga kuhusishwa kwa Urusi na uchaguzi mkuu uliopita.
-
Mtanzania akamatwa na dawa za kulevya India
-
Uchumi wa Korea Kaskazini wazidi kuimarika
-
Marekani yaridhia kuiwekea vikwazo Urusi
-
Trump aungana na bunge kuiwekea vikwazo Urusi
Hata hivyo, Mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya kimataifa ya bunge la Urusi, Duma Leonid Slutsky amesema kuwa kama Marekani itachukua hatua hizo mpya basi itakuwa imezorotesha uhusiano baina ya Urusi na Marekani