Waziri wa Fedha wa Marekani, Steve Mnuchin ametoa onyo kali kwa mataifa yanayoshirikiana kibiashara na Korea Kaskazini kwamba yanafanya hivyo kwa kujiweka katika nafasi ngumu zaidi.

Ameyasema hayo wakati akitangaza vikwazo vipya dhidi ya kampuni yoyote duniani inayosaidia kufadhili mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini na kwamba itapoteza haki ya kufanya biashara na Marekani.

Amesema kuwa Marekani kwasasa huenda ikaanza kusimamisha na kupekua meli zinazo safirisha mizigo kupeleka Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini tayari inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa kupitia Umoja wa Mataifa pamoja na vile vya Marekani kuhusu mpango wake wa Kinyuklia.

Hata hivyo, Marekani imesema kuwa vikwazo vipya vinalengo la kuidhibiti zaidi Korea Kaskazini, kwa njia ya kukata vyanzo vyake vya fedha na nishati ili kukomesha programu yake ya nyuklia.

Mourinho adai anasubiri muda ufike achukue pointi tatu kwa Chelsea
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 25, 2018