Seneta wa California Kamala Harris Mgombea mwenza wa Urais kupitia chama cha Democrat kwa mara ya kwanza ametokea kwenye kampeni za Urais za Joe Biden ambapo amemkosoa Rais aliyepo madarakani Donald Trump kwa kushindwa kulikabili vilivyo janga la corona.

Amesema kuwa taifa la Marekani limeingia hatarini kwa kushindwa kuweka umakini katika kukabiliana na janga la corona na kuiingiza nchi hiyo kwenye mzozo wa kiuchumi huku bado ikiwa inapambana na kukosekana kwa usawa wa rangi na kijamii.

“Huu ni wakati wa matokeo halisi kwa marekani kila kitu kilicho muhimu kwetu, uchumi wetu, afya, watoto wetu na aina ya taifa tunalosihi, kila kitu kipo kwenye mstari. Tupo katika mzozo mbaya kabisa wa kiafya wa karne. Raisi ameshimdwa kushugulikia janga hili na kututumbukiza kwenye mzozo mbaya kabisa wa kiuchumi kuwahi kutokea tangu mgororo mkubwa kabisa wa kiuchumi”. Amesema Kamala.

Aidha Joe Biden amesema serikali yake na Harris itakuwa na mkakati thabiti wa kukabiliana na COVID 19 utakao badilisha hali ya mambo uvaaji wa barakoa, kuongeza upimaji na kuziwezesha serikali za majimbo ili kufungua shule na biashara kwa usalama.

Harris awataka wamarekani kutumia fursa waliyonayo kufanya maamuzi.

Mgodi wa GGML kuinufaisha Geita
Vijana watakiwa kushiriki shughuli za kijamii