Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson yuko mjini Beijing kufanya mazungumzo na viongozi wa China huku ajenda kuu katika mkutano huo ikiwa ni mzozo katika rasi ya Korea.

Utawala wa Trump unaamini China ina umuhimu mkubwa, katika juhudi za kuishurutisha Korea Kaskazini kusitisha uundaji wa silaha zake za nyuklia.

Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni na China imeonyesha kujitolea kwake katika utekelezaji wa vikwazo vya umoja wa mataifa dhidi ya taifa hilo.

Siku ya Alhamisi, Beijing ilitangaza kuwa mashirika ya Korea Kaskazini yanayoshirikiana na China hayana budi kufungwa.

Ziara ya Tillerson nchini China inakuja huku rais Trump akitarajiwa kutembelea taifa hilo baadaye mwezi Novemba mwaka huu.

Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 1, 2017
Video: Harry Kane azidi kuing'arisha Spurs