Marekani na Korea Kusini zimefanya mazoezi makubwa ya pamoja ya kijeshi mapema hii leo Oktoba 19, 2022 yaliyojumuisha wanajeshi karibu 1,000, vifaa vya kijeshi pamoja na ndege za kijeshi katika eneo la Yeoju.

Kamanda wa kikosi kilichoshiriki mazoezi, Kapteni Sean Kasprisin amesema mazoezi hayo yanalenga kuthibitisha uwezo wa kijeshi wa vikosi vya Marekani na Korea.

Silaha za kivita. Picha: Defence News.

Mapema hii leo Jumatano, Korea Kaskazini ilifyatua makombora kuelekea Bahari ya Kaskazini, ili kujibu mazoezi hayo ya kijeshi ya Korea Kusini kwenye eneo la mpaka wakati mahasimu hao walishutumiana kwa kuchochea wasiwasi katika Rasi ya Korea kwa majaribio ya silaha.

Hata hivyo wanadiplomasia bado hawajatoa kauli zao juu ya atukio hayo ingawa taarifa za awali zinasema hali hiyo inaashiria kutunushiana misuli baina ya mataifa hayo yenye nguvu Duniani.

Rais Samia akutana na Malkia Maxima
Mapigano yapamba moto, wananchi wasema wanamuachia Mungu