Ubalozi wa Marekani nchini Iraq umewataka raia wake wote wanaoishi Iraq kuondoka nchini humo mapema iwezekanavyo kutokana na kuongezaka kwa mvutano na vurugu nchini Iraq.

Jumanne iliyopita Waandamanaji walifanikiwa kuvunja ukuta wa Ubalozi huo na kuwasha moto ndani ya Ubalozi ikiwa ni hasira zilizosababishwa na Marekani kuwaua Wapiganaji 24 wanaoungwa mkono na Iran wiki liyopita.

Ubalozi huo umesema, kutokana na Waandamanaji kuendelea kuzingira Ubalozi, huduma zinasitishwa kwa muda usiojulikana na Raia wa Marekani wanatakiwa kutosogea karibu na Ubalozi na wananchi wanaotaka kusafiri kwenda huko wasitishe.

Aidha, mapema leo Rais Trump ametoa amri ya kumuua Kiongozi wa Kikosi cha Quds cha Iran, Qasem Soleimani akiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad, hatua iliyopingwa Spika Nancy Pelosi.

Kiongozi wa Kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei amesema kisasi kikali kitalipizwa kwa waliohusika na kumwaga damu za wenzao huku Waziri wa Mambo ya Nje, Javad Zarif akisema ni Uchochezi.

Kabendera atuma Barua kwa waombolezaji msiba wa mama yake
DC Tunduru apiga marufuku sherehe za wazazi kwa wanaohitimu darasa la saba