Marekani na kundi la Wanamgambo wa Taliban, wameanza mazungumzo mapya jijini Doha nchini Qatar kwaajiri ya kufikia makubaliano ya kusitisha mashambulizi yanayofanywa na kundi hilo.
Msemaji wa Wanamgambo wa Taliban amesema hayo wakati ambapo Marekani ikitarajia kupatikana maelewano, kabla ya uchaguzi wa rais wa Afghanistan utakaofanyika Septemba mwaka huu.
Aidha, msemaji huyo wa Wanamgambo wa Taliban, Zabiullah Mujahid ameandika kwenye ukurasa wa Twitter kuwa awamu ya saba ya mazungumzo na wawakilishi wa Marekani pamoja na timu ya washauri wa Kiislamu wa Emirati imeanza mazungumzo jijini Doha.
Amesema kuwa mazungumzo hayo yanalenga kumaliza vita vya muda mrefu zaidi vya Marekani Afghanistan ambapo Wanamgambo hao wanataka Marekani iondoe majeshi yake nchini humo.
Hata hivyo, mazungumzo hayo yameanza katika mji wa Doha nchini Qatar wakati ambapo taarifa zimesema Taliban imewaua wanamgambo 25 wanaounga mkono serikali ya Afghanistan katika shambulizi walilolifanya Kaskazini mwa Afghanistan.
-
Marekani yaanza mazungumzo na Wanamgambo wa Taliban
-
Trump, Kim Jong Un wateta kimyakimya
-
Mgogoro wa China na Marekani waanza kupoa, Trump aruhusu bidhaa za Huawei Marekani