Marekani imeendeleza ubabe wake wa kuzitungua ndege za kijeshi za Syria mara baada ya kuitungua ndege nyingine kusini mwa nchi hiyo, tukio hilo limekuja siku chache zilizopita kutungua ndege nyingine ya nchi hiyo.
Aidha, Marekani inadai kuwa ndege hiyo iliyotunguliwa ya Jeshi la Syria ilikuwa imebeba silaha nzito na hatari kwa Jeshi la Marekani la ardhini hivyo imechukua hatua hiyo kwaajili ya kujikinga na hatari ya kushambuliwa.
Katika hatua nyingine, Jeshi hilo la Marekani limedai kuwa limemuua kiongozi wa ngazi za juu wa wanamgambo wa Islamic State ambao wakiwashambulia mara kwa mara ili kuweza kurudisha hali amani katika nchi hiyo ya Syria.