Marekani imeidhinisha chanjo ya virusi vya corona iliyotengezwa na kampuni ya Moderna kuanza kutumika kwa dharura.

Mamlaka ya kusimamia usalama wa chakula na dawa FDA, imeidhinisha matumizi ya chanjo hiyo ya pili ili kuongeza juhudi za kumaliza janga la Corona nchini Marekani.

Chanjo ya Moderna itatumika katika maeneo ambayo ni vigumu kufikiwa kwasababu ya urahisi wa kuhifadhi chanjo hiyo.

Kamishna wa Mamlaka ya chakula na dawa Stephen Hahn amesema kupatikana kwa chanjo mbili ni hatua kubwa katika kukabiliana na idadi kubwa ya maambukizi na vifo kutokana na janga la Corona.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Donald Trump ametoa pongezi kwa kampuni ya Moderna kwa kuharakisha upatikanaji wa chanjo hiyo.

Wakati huo huo rais mteule wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kupatiwa chanjo ya kwanza ya COVID-19 Jumatatu ya wiki ijayo.

Majaliwa aipa TPA wiki 2 Bandari ya Kagunga itoe huduma
Baba Jokate afariki dunia