Mkurugenzi Tume ya Haki za Binadamu (KHRC), George Kegoro, Serikali ya Marekani na Baraza la Maaskofu wamepinga vikali harakati zinazoendela jijini Nairobi, Kenya kufuatia hatua zilizochukuliwa na Serikali kukiuka amri ya mahakama kuvifungulia vituo vya Televisheni vilivyofungiwa baada ya kurusha tukio la Raila Odinga la kujiapisha kama Rais wa watu nchini humo.
Kufuatia hatua hiyo ya Serikali, wananchi nchini humo wameandamana wakishinikiza kuondolewa kwa amri hiyo ya kuvifungia vituo hivyo vya televisheni vilivyofungwa January 30.
Ambapo maandamano hayo yalivurugwa na kusambaratishwa na polisi kwa kutumia mabomu ya machozi.
Mkurugenzi wa Tume ya Haki za Binadamu KHRC, George kegoro amesema anapata wasiwasi juu ya kile alichoita kutoheshimu sheria.
-
Video: Maajabu mazishi ya Kingunge, Sheikh atangaza kumshtaki Mange Kimambi kwa Mungu
-
NEC yafunguka kuhusu uchaguzi Kinondoni
”Tupo hapa sote kama ishara ya mshikamano .. Hii haikubaliki, kufungwa vituo vitatu vya televisheni. Haikubaliki ..Hiki ndichi kilitustua. Tunapinga hili ,”amesema Kegoro.
Licha ya amri ya mahakama iliyotaka serikali kuondoa zuio kwa vituo hivyo vya Televisheni , Serikali imeshikilia msimamo wa kutovifungulia vituo hivyo ni KTN News, Citizen, NTV, Inooro TV na Radio Citizen.
Wanaharakati walikuwa wakijaribu kuyafikia majengo ya ofisi za Serikali katikati mwa Nairobi polisi walifyatua mabomu ya gesi.
Hivyo Serikali ya Marekani inahisihi Serikali ya Kenya kuruhusu vituo vya Televisheni kufunguliwa kwani uhuru wa vyombo vya habari ni muimu sana hakuna budi kuzingatia katiba na utawala wa sheria kwani Amri za mahakama zinapaswa kuheshimiwa.