Marekani imeamua kuingilia kati mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini Ethiopia kwa kumtuma Waziri wa Mambo ya Nje, Rex Tillerson.
Kwa mujibu wa gazeti la Addis Standard la Ethiopia, Ubalozi wa Marekani umesema Tillerson ataingia nhini humo kufanya mazungumzo na Serikali Machi 7 mwaka huu na kwamba imeipa umuhimu mkubwa hali ya kisiasa nchini humo.
“Hali ya mgogoro wa kisiasa nchini Ethiopia itachukua nafasi kubwa katika majadiliano na maafisa wa Serikali ya nchi hiyo,” chanzo cha ubalozi huo kimeelza.
Hatua hii inachukuliwa kama utekelezaji wa ahadi ya Rais Donald Trump kupitia barua yake kwa viongozi wa Afrika katika mkutano wa Umoja wa Afrika Januari mwaka huu kuwa atamtuma Tillerson kufanya ziara barani Afrika.
Hivi karibuni, Serikali ya Ethiopia ilitangaza hali ya hatari nchini humo kutokana na kuzuka taharuki ya kisiasa inayotokana na madai ya chama kikuu cha upinzani cha Ethiopia Peoples’ Revolutionary Democratic Front (EPRDF) kinachotaka kufanyika mabadiliko ya kimfumo.
- Video: Mnyika awaweka kwenye mzani Dkt Slaa na Dkt Mashinji, ‘ni usaliti’
- Video: Nitashtaki kwa Mungu- Mama ‘Sugu’, Maaskofu TEC wajilipua
Chama hicho kimetaka wafungwa wa kisiasa kuachiwa huru na kuitisha maandamano. Serikali imewaachia baadhi ya wafungwa wa kisiasa lakini bado hali imeendelea kuwa tete na madai ya kuwaachia wengine yameendelea.