Marekani imefanya shambulizi la anga kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani dhidi ya wapiganaji wa Kikundi cha Islamic State nchini Somalia na kusema imepiga hatua ya kipekee katika vita hiyo.

Marekani imeendelea kuwashambulia wapiganaji wa jihadi kutoka katika kikundi cha waasi cha al-Shabaab ambacho kinamafungamano na al-Qaeda, lakini yaliyotokea Ijumaa ni hatua kubwa iliyofikiwa kutokana na kuendelea kwa vita hii dhidi ya IS.

“Majeshi ya Marekani yataendelea kutumia njia zote zinazokubalika na mwafaka kulinda Wamarekani na kuvidhoofisha vikundi vya kigaidi,” AFRICOM imesema.

Aidha, hii ni mara ya kwanza kwa Marekani kushambulia kikundi hicho katika nchi ya Pembe ya Afrika, hivyo huu ukiwa ni muendelezo wa kupambana na vikundi vya ugaidi duniani ambavyo vimekuwa ni tishio kwa usalama.

Hata hivyo, Msemaji wa kikosi cha AFRICOM Luteni Kamanda, Anthony Falvo amesema hakuna raia waliokuwa karibu na eneo hilo lililokuwa limeshambuliwa, hivyo hakuna madhara yeyote yaliyotokea.

Kante kuibeba Chelsea leo?
Magazeti ya Tanzania leo Novemba 5, 2017