Balozi maalumu wa Marekani  Korea Kaskazini amesema kuwa Marekani inafikilia kuanzisha mashambulizi ya kutumia silaha wa kipekee katika kuiadhibu Pyongyang kwa kufanya jaribio la Kinyuklia.

Balozi Sung Kim, amesema hii itakuwa pamoja na hatua zinazopangwa kuchukuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa.

Aidha bwana Kim, ambaye amekuwa akikutana na maafisa wa Serikali jijini Tokyo alisema kuwa Marekani pia inapanga mikakati mingine kwa ushirikiano na Japan na Korea Kusini kuweza kuiadhibu korea ya kaskazini kwa mpango wake wa kuendelea kukaidi maagizo ya baraza la umoja wa mataifa kuhusu silaha za nyuklia ambazo zinapingwa duniani kote.

Marekani Yaadhimisha Shambulio La Septemba 11
Shambulio La Kigaidi Latokea Katika Kituo Cha Polisi Mjini Mombasa na Kujeruhi Askari Kadhaa, Ulinzi Waimarishwa