Nchi ya Marekani ambayo ndiyo mfadhili mkubwa wa WHO anayetoa ufadhili wa kiasi cha dola milioni 400 ambayo ni 15% ya bajeti yake ya mwaka jana imesitisha ufadhili kwa shirika hilo.
Rais wa Marekani , Donald Trump amesema kuwa uongozi wake utasitisha ufadhili kwa Shirika la afya duniani (WHO) kwakuwa limeshindwa kufanya majukumu yake muhimu katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.
“Ninawapa muongozo utawala wangu kusitisha ufadhili wakati Shirika la afya duniani likiwa linachunguzwa katika majukumu yake yaliyoshindwa kuyatimiza katika kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona ,” Trump aliwaambia waandishi katika White House.
Wakti hayo yakijiri ikumbuke kuwa, Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani kwa kuwa na wagonjwa 608,377 na vifo vilivyotokana na ugonjwa huo kufikia 25,981.
WHO, ilitenga kiasi cha dola milioni 675 kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na limeripotiwa kuwa litaongeza fedha hizo hadi karibu dola bilioni moja.
WHO kutafiti sababu waliopona Corona kuumwa tena
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa António Guterres alisema kuwa wakati huu si wakati wa kukata ufadhili kwa WHO.