Serikali ya Marekani imesema haina mpango wakutoa msaada wa kijeshi “wakati huu”
Taarifa hiyo imekuja baada ya nchi ya Haiti Kuomba Marekani na Umoja wa Mataifa (UN) vikosi vya kigeni kutumwa nchini humo kulinda miundo mbinu muhimu ya nchi hiyo baada ya kuuawa kwa Rais Jovenel Moïse.
Ijapokuwa Marekani haitatoa msaada wa kijeshi, siku ya Ijumaa imesema itawapeleka maafisa shirika la upepelelezi la FBI na wale wa usalama wa kitaifa nchini Haiti kusaidia kwa kuchunguza.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatakiwa kuidhinisha mpango wa kupelekwa kwa vikosi vya kimataifa nchini Haiti chini ya udhamini wa UN.
Awali polisi wa Haiti wamesema kundi la mamluki 28 wa kigeni walihusika na mauaji ya rais siku ya Jumatano na baada ya makabiliano makali ya bunduki 17 kati yao walikamatwa.
Polisi wamesema Baadhi ya wanachama wa kundi hilo ambalo Haiti inasema ni pamoja na wanajeshi wastaafu wa Colombia, walizuiliwa katika nyumba waliokuwa wakitumia, baada ya wengine kuingia makazi ya kidiplomasia ya Taiwan, Kati yao Washukiwa watatu waliuawa na polisi, na wengine wanane wanatafutwa.
Hali ya hatari imeendelea kudumishwa kote nchini humo na kwa sasa haijulikani ni nani anaongoza serikali.
Shambulio dhidi ya makazi ya Rais yalifanyika usiku wa Julai 7, wakati wanaume waliojihami walipovamia makazi ya Rais, kumpiga risasi na kumuua na kumjeruhi mke wake. , aliyepatikana na majeraha 12 ya risasi.
Kulingana mamlaka Bado haijabainika ni nani aliyepanga shambulio hilo na lengo lake.