Marekani imewaonya wanaokiuka makubaliano ya usitishaji mapigano ya Sudan watawajibishwa kwani hivi karibuni pande mbili zinazozozana zilishindwa kutekelezwa saa kadhaa za kusitisha mapigano baada ya kuanza upya kurushiana silaha.

Onyo hilo, limetolewa na Marekani kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya Nje, Antony Blinken ambaye amesema makubaliano ya usitishaji mapigano ya Sudan ya hivi karibuni kati ya pande mbili zinazozozana yalishindwa kutekelezwa.

Wawakilishi wa jeshi la Sudan na vikosi hasimu vya wanajeshi wa akiba walikuwa walikubaliana kusitisha mapigano kwa siku saba ili kuruhusu kuanzishwa tena kwa huduma muhimu na misaada ya kibinadamu.

Makubaliano mapya zaidi ya sasa ya kusitisha mapigano yaliyotiwa saini na pande mbili zinazopigana za Sudan yalitokana na juhudi za diplomasia, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, alisema Jumanne kupitia Twitter.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 25, 2023
Man City kuibania Arsenal usajili wa Gundogan